久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Teknolojia za kisasa na za kijani zavutia ufuatiliaji mkubwa kwenye Maonyesho ya China-ASEAN (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 27, 2024
Teknolojia za kisasa na za kijani zavutia ufuatiliaji mkubwa kwenye Maonyesho ya China-ASEAN
Gari linalotumia nishati ya umeme likionyeshwa kwenye Maonyesho ya 21 ya China na Nchi za Jumuiya ya Asia Kusini Mashariki (ASEAN) mjini Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Septemba 26, 2024. (Xinhua/Zhang Ailin)

NANNING – Ikiongozwa kwa udhibiti wa mbali, mashine ya kupakia mizigo inaweza kupakia nyenzo zenye uzito wa tani nyingi au hata kuzisafirisha hadi kwenye sehemu za uzalishaji bidhaa — ambapo kazi zote hizi hufanywa bila dereva nyuma ya usukani. Mashine hii ya kutumia teknolojia za kisasa, iliyoundwa na kuzalishwa na Kampuni ya Kuunda Mashine ya Guangxi LiuGong ya China, ni baadhi tu ya teknolojia nyingi za kijani ambazo zinafuatiliwa sana kwenye Maonyesho yanayoendelea ya China na Nchi za Jumuiya ya Asia Kusini Mashariki (ASEAN).

"Ikitilia maanani mahitaji ya bidhaa za hali ya juu, za aina mbalimbali, na zenye umaalum kwa wateja katika soko la mashine za ujenzi, kampuni hiyo ya LiuGong imezingatia uwekaji wa teknolojia za kielektroniki, kidijitali, mtandao na za akili mnemba kwenye mashine, ikiwa na ukuaji wa kila mwaka tarakimu mbili katika uwekezaji wa R&D," amesema Li Dongchun. meneja mkuu wa kampuni hiyo.

Katika Maonyesho ya China na ASEAN yanayoendelea huko Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, kampuni hiyo ya kutengeneza mashine za ujenzi inaonyesha bidhaa nane za kielektroniki, zikiwemo mashine za kupakia, kuchimba na kubeba mizigo ili kuitikia mahitaji yanayoongezeka ya bidhaa za kisasa na kijani zinazozalishwa na kampuni za China katika nchi za ASEAN.

Biashara ya China na nchi za ASEAN imekuwa ikirekodi ukuaji thabiti kwa miaka mingi. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa ASEAN kwa miaka 15 mfululizo, na thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka kutoka yuan bilioni 876.4 (dola za kimarekani kama bilioni 124.6) Mwaka 2004 hadi yuan trilioni 6.41 Mwaka 2023, ikiwa ni wastani wa asilimia 11 ya ukuaji wa kila mwaka.

Wakati ambapo China iko inaongeza juhudi za kuhimiza vichocheo vipya vya ukuaji wa uchumi vyenye kutumia teknolojia ya hali ya juu na rafiki kwa mazingira, bidhaa na teknolojia hizo za kisasa na kijani zinavuta hisia za waonyeshaji bidhaa na watembeleaji katika maonyesho hayo.

Hafla ya utiaji saini kwenye maonyesho hayo siku ya Jumanne wiki hii ilishuhudia mikataba 109 ikitiwa saini, ikihusika na sekta ibuka za kimkakati kama vile nishati mpya, viwanda vya teknolojia za hali ya juu na taarifa za kielektroniki.

Kao Kim Hourn, katibu mkuu wa ASEAN amesema, China na nchi za ASEAN zinatafuta fursa mpya za ushirikiano katika nyanja kama vile akili mnemba na nishati safi, ili kuendeleza malengo ya pamoja ya uvumbuzi na maendeleo endelevu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>