Lugha Nyingine
Kituo cha Maonyesho ya AI ya “Mahali kama Ndoto” kilichojengwa na People’s Daily Online chafunguliwa Nanning, Mkoa wa Guangxi, China
Picha hii ikionyesha Kituo cha Maonyesho ya Akili Mnemba ya “Mahali kama Ndoto” ambacho kimezinduliwa na kuanza kutumika. (Picha na Yan Lizheng/People’s Daily Online) |
Kituo cha Maonyesho ya Akili Mnemba ya “Mahali kama Ndoto” cha Kampuni ya People's Daily Online na Shirika la Maendeleo ya Utalii la Guangxi kimezinduliwa na kuanza kutumika rasmi Septemba 25, siku ya Jumatano mjini Nanning, Mkoa wa Guangxi, China.
Kituo hicho ambacho kimefunguliwa kwa mara ya kwanza mkoani humo kimeshuhudia mfululizo wa ushirikiano na mafanikio mapya ya "Biashara ya Mtandaoni kando ya Njia ya Hariri": Umoja wa kwanza wa Ushirikiano wa Kikanda wa Biashara ya Mtandaoni nchini China ulitangazwa, mikoa, miji na maeneo 12 ya Magharibi mwa China yalitia saini “Makubaliano ya Maelewano (MoU) ya Umoja wa Ushirikiano wa Biashara ya Mtandaoni", hatua za kuunga mkono kampuni kushiriki jukwaa la “Biashara ya Mtandaoni kando ya Njia ya Hariri” zimetangazwa kwa umma kwa mara ya kwanza.
Kituo cha Maonyesho ya Akili Mnembaa “Mahali kama Ndoto” kimejengwa kwa pamoja na Kampuni ya People’s Daily Online na Shirika la Maendeleo ya Utalii la Guangxi na kinapatikana kwenye Makumbusho ya Mipango ya Guangxi.
Baada ya hafla ya uzinduzi, viongozi na washiriki waliokuwa kwenye hafla hiyo walitazama tamthilia ya kwanza ya Akili Mnemba "Safari ya kiajabu ya Baize" iliyoandaliwa na People's Daily Online kwa kujitegemea.
Shughuli mfululizo za ushirikiano pia zimepata mafanikio katika hafla hiyo: Kampuni tano zimetia saini mikataba ya ushirikiano wa kimkakati wa AI+; kundi la kwanza la washirika wa Mpango wa ushirikiano wa AI+ wa “Mahali kama Ndoto” wa People's Daily Online na Shirika la Maendeleo ya Utalii la Guangxi lilitia saini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma