Lugha Nyingine
Ujumbe wa Waandishi wa Habari wa nchi za Latin Amerika wafurahia kuchuma na kuonja chai huko Chengdu, China
Waandishi wa habari wa ujumbe wa vyombo vya habari vya nchi za Latin Amerika wakijaribu kuchuma chai. (Picha na Wang Xiaoxia/People’s Daily Online) |
Ujumbe wa vyombo vya habari vya nchi za Latin Amerika unaojumuisha waandishi wa habari kutoka Argentina, Brazil, Colombia, Peru na nchi nyingine ulikwenda kwenye Maskani ya Chai ya Chengjia yaliyopo Wilaya ya Pujiang, Mji wa Chengdu katika Mkoa wa Sichuan, China siku ya Jumatatu Septemba 23, ili kujionea na kujaribu shughuli za uchumaji, uandaaji na uonjaji chai na maisha mengine ya kipekee ya utamaduni wa chai.
Maskani ya Chai ya Chengjia pia yanajulikana kwa jina la mji mdogo wa Chengjia uliopo Wilaya ya Pujiang. Mji huo mdogo, una hali ya umande mwingi, ukungu mzito na unyevu mwingi, na misitu iliyostawi, ambayo ni mwafaka kwa uzalishaji wa klorofili ya chai na harufu yake nzuri. Unafurahia hadhi ya kuwa “Maskani Bora Zaidi ya Chai ya Kijani ya China.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma