Lugha Nyingine
Mji wa Kashgar wa Xinjiang, China wageuka kuwa eneo la kipekee la watalii linalochanganya historia na mambo ya kisasa (3)
Wakazi wenyeji wakifurahia muda wao wa mapumziko katika mji wa kale wa Kashgar, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kusini magharibi mwa China, Septemba 19, 2024. (Xinhua/Zhao Yusi) |
Mji wa kale wa Kashgar, ulioko Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kusini magharibi mwa China, ulitumika kama kituo muhimu cha usafirishaji kilichounganisha China na Asia ya Kati na Asia Kusini katika zama za kale. Kukutana kwa tamaduni mbalimbali za kikabila katika eneo hilo kumeleta kuongezeka kwa hazina nyingi za kihistoria na kitamaduni.
Kwa sasa, mji huo wa Kashgar umetumia faida zake za kitamaduni na kijiografia, ukigeuka kuwa kivutio cha kipekee cha watalii kinachochanganya historia na mambo ya kisasa.
Katika miezi minane ya kwanza ya Mwaka 2024, mji huo ulipokea watalii wa ndani zaidi ya milioni 19.5, ongezeko la asilimia 29.46 mwaka hadi mwaka, na kuzalisha mapato ya utalii yanayofikia yuan karibu bilioni 15.35 (dola za Kimarekani kama bilioni 2.18), ikiwa ni ongezeko la asilimia 38.83.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma