Lugha Nyingine
Habari picha: Mrithi wa sanaa ya uchongaji vinyago vya magogo ya Wuyuan Mashariki mwa China (6)
Picha hii ikionesha sehemu ya kazi ya vinyago vya kuchongwa kwenye magogo katika Kijiji cha Wangkou cha Wilaya ya Wuyuan, Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China Septemba 20, 2024. (Xinhua/Wan Xiang) |
"Uchongaji Vinyago wa Aina Tatu wa Wuyuan" unajumuisha Sanaa za uchongaji kwenye mawe, matofali na magogo, kati yao uchongaji vinyago kwenye magogo ni wenye uwakilishi zaidi wa Sanaa za uchongaji za Wuyuan. Ukiwa unajivunia historia ya zaidi ya miaka 1,000, ufundi huo wa kuchonga vinyago uliorodheshwa kuwa urithi wa utamaduni usioshikika wa China Mwaka 2006.
Uchongaji wa vinyago kwenye magogo wa Wuyuan unajikita katika kuonyesha usanifu wa sehemu maalum za majengo ya ujenzi wa mtindo wa Huizhou kama vile nguzo na fremu za dirisha. Mbinu mbalimbali zinatumiwa katika kuchonga picha za kupendeza za miundo yenye kuvutia ya China, ikionyesha uthamini endelevu wa uzuri na matarajio ya watu juu ya maisha bora.
Yu Youhong, mrithi wa ufundi huo, pia amejitolea kulinda na kukarabati majengo ya kale katika mji wake huo alikozaliwa. Hivi sasa, Yu na wanafunzi wake wamekarabati na kurejesha sura ya vinyago vya magogo kwenye majengo ya kale zaidi ya 100 yaliyojengwa katika enzi za Ming na Qing (1368-1911).?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma