Lugha Nyingine
Matunda ya matufaha yaning'inia kwa wingi matawini mkoani Shaanxi, China huku wakulima wakifurahia mavuno (3)
Matunda ya matufaha ya rangi nyekundu yakining'inia kwenye matawi mwezi huu wa Septemba.(People’s Daily Online/Sun Ting) |
Mwezi Septemba mwaka huu matunda ya matufaha ya rangi nyekundu yameanza kuning'inia kwa wingi kwenye matawi ya miti katika wilaya ya Baishui ya Mji wa Weinan, Mkoa wa Shaanxi nchini China, ikiashirikia kuiva na kuanza kuchumwa kwa matunda hayo, hali inayoleta furaha kwa wakulima wenyeji.
Katika miaka ya hivi karibuni, wakulima wa eneo hilo wameweza kutumia mbinu za upandaji wa kisayansi na kudhibiti ubora kwa makini, hali ambayo imefanya matunda hayo ya matufaha ya Baishui kufuatiliwa na kuuzwa vizuri kwenye soko.
Tangu miaka ya 1980, wilaya hiyo ya Baishui, ilianza kuendeleza tasnia ya matufaha. Kwa sasa, matufaha ya Baishui yamekua tasnia ya kuongeza kipato kwa wananchi.
Inafahamika kuwa, wilaya ya Baishui ina eneo la upandaji matufaha lenye ukubwa wa hekta 20, 000, na imekuwa kituo kikuu cha biashara ya usambazaji matufaha katika eneo la kaskazini-magharibi mwa China. Mwaka 2023, Wilaya ya Baishui iliuza matufaha yenye uzito wa zaidi ya tani Milioni 2, yakiwa na thamani ya uzalishaji wa awali wa yuan bilioni 5.2 na thamani ya jumla ya mnyororo wa tasnia nzima ya yuan bilioni 11.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma