Lugha Nyingine
Habari?picha: Mwalimu wa darasa la Opera ya Kunqu katika Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China (2)
Akiwa alizaliwa mwaka 1995 na kukulia katika Mji wa Kunshan Mkoani Jiangsu, Mashariki mwa China, kumbukumbu za utotoni za Zhou Jie zimejaa Opera ya Kunqu kwenye kila sikukuu na sherehe.
Mji wa Kunshan ni mahali pa kuanzia kwa Opera ya Kunqu, ambayo imeorodheshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuwa urithi wa utamaduni usioshikika. Mji huo ulianzisha "darasa la mafunzo ya Opera ya Kunqu" katika shule moja ya msingi Mwaka 1992. Kwa sasa, kuna madarasa zaidi ya 20 ya kufundisha opera ya Kunqu mjini humo, huku wanafunzi zaidi ya 5,000 wakiwa wamefunzwa.
Mwaka 2021, Zhou Jie, mwigizaji wa zamani wa Opera ya Kunqu, alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi ya Shipai ya Kunshan, akiongoza wanafunzi kucheza Opera ya Kunqu.
Akizungumzia siku za baadaye, kijana huyo anatumai kuwa watoto wengi zaidi wataweza kuja kujifunza na kufurahia utamaduni wa Opera ya Kunqu, na kurithisha urithi huu wa utamaduni usioshikika kwa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma