Lugha Nyingine
Waziri wa mambo ya nje wa China asema mkutano wa kilele wa FOCAC wa 2024 umepata "mafanikio mazuri " (3)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya Alhamisi alipokutana na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Yacine Fall na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kongo Jean-Claude Gakosso amesema kuwa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) umepata mafanikio mazuri.
Akifafanua kuhusu matokeo makubwa ya mkutano huo, Wang amesema uhusiano wa pande mbili kati ya China na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kibalozi na China umepandishwa hadhi hadi kwenye ngazi ya uhusiano wa kimkakati.
Uelezeaji wa jumla wa sifa ya uhusiano kati ya China na Afrika umeinuliwa kuwa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya na katika hali yoyote, amesema Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
Mapendekezo sita makubwa ya kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na Afrika yametolewa, Wang amesema.
Mpangokazi wa hatua za kuendeleza ushirikiano kati ya China na Afrika umewekwa, amesema, akiongeza kuwa Rais Xi Jinping wa China ametangaza hatua 10 za ushirikiano kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa ili kuzidisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo.
Katika mkutano huo, China na Afrika zimekubaliana kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi yao ya msingi na kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi. Pia zimekubaliana kupinga maoni ya upande mmoja, kushughulikia hali isiyo na haki na usawa ya kihistoria na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa ili kuufanya unufaishe watu wote, Wang amesema.
Mkutano huo kilele umeonyesha imani thabiti ya Nchi za Kusini katika mshikamano na ushirikiano, Wang amebainisha.
Kwa upande wake Fall na Gakosso wamesema, ushirikiano wa Afrika na China umebadilisha mustakabali wa Afrika na bila shaka utaingia katika historia kama mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa kimataifa.
Afrika inapenda kufanya kazi na China katika kutekeleza matokeo ya mkutano huo na makubaliano kati ya pande hizo mbili, kuimarisha urafiki kati ya Afrika na China, na kufikia maendeleo na ustawi kwa pamoja, wamesema.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma