Lugha Nyingine
Marais wa China na Afrika Kusini?watangaza kuinua hadhi?ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili (5)
Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na ziara ya kiserikali, katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mkutano wao mjini Beijing, China, Septemba 2, 2024. (Xinhua/Yao Dawei) |
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na ziara ya kiserikali siku ya Jumatatu wametangaza kupandisha hadhi ya uhusiano kati ya pande mbili kuwa ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kwa pande zote katika zama mpya.
Rais Xi amesema kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini kunaendana na matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili na mchakato wa kihistoria wa maendeleo ya Nchi za Kusini.
Rais Xi ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuongoza uhusiano wa pande mbele kusonga mbele kwa hali ya kuaminiana kimkakati katika ngazi ya juu na amesisitiza kufanya juhudi za pamoja ili kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu wa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuboresha ushirikiano katika uchumi wa kidijitali, akili bandia na nishati mpya, na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika maendeleo ya rasilimali watu.
Rais Xi amesema China itafungua mlango yake kwa nchi za Afrika, na kuongeza kuwa nchi hiyo ingependa kushirikiana na Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika ili kuanzisha ari na kasi mpya ya ushirikiano na kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya ushirikiano kati ya China na Afrika.
“Kadiri hali ya kimataifa inavyozidi kuwa ngumu, ndivyo nchi za Kusini zinavyopaswa kudumisha kujiamuliwa, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, na kulinda kwa pamoja haki na usawa wa kimataifa,” Rais Xi amesema.
Kwa upande wake Ramaphosa amesema Afrika Kusini itaendelea kuwa rafiki wa kuaminika na wa kutegemewa wa China.
Kwa kutumia fursa ya kujenga ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kwa pande zote katika zama mpya, Afrika Kusini itapanua na kuimarisha ushirikiano wenye matokeo halisi na China katika sekta za uchumi, biashara, uwekezaji, miundombinu, nishati mpya na kupunguza umaskini. Pia itaongeza mawasiliano kati ya watu na ushirikiano wa elimu na utamaduni na China, Rais Ramaphosa amesema.
Rais Ramaphosa ameongeza kuwa ushirikiano chini ya mfumokazi wa FOCAC umeleta manufaa makubwa kwa nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma