Lugha Nyingine
Wanandoa wa Rwanda waendelea na masomo?ya teknolojia ya Juncao katika Mkoa wa Fujian, China
Juncao ni nyasi chotara na rasilimali muhimu ya kilimo yenye matumizi mengi iliyoendelezwa na kutumika kwa kilimo cha uyoga nchini China. Ikiwa ilibuniwa na Lin Zhanxi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian (FAFU) katika miaka ya 1980, teknolojia ya Juncao imenufaisha nchi zaidi ya 100, ikiwemo Rwanda, ikiwezesha wakulima wadogo kulima uyoga kutoka kwenye nyasi zilizokatwa na kukaushwa, bila kukata miti na kuharibu mazingira.
Hatungimana Mediatrice, mratibu wa mradi wa Juncao nchini Rwanda, alisoma shahada ya uzamili ya vimelea katika biolojia Mwaka 2017 katika chuo kikuu cha kilimo na Misitu cha Fujian. Mwaka uliofuata, mume wake Nsanzinshuti Aimable alijiunga naye kusoma na kuishi Fujian. Chini ya usimamizi wa Profesa Lin Zhanxi, Mediatrice na Aimable wamefanikiwa kupata shahada zao za uzamili. Ili kuwa na ufahamu wa kina wa teknolojia ya Juncao, wanandoa hao wa Rwanda wamechagua kuendelea kubaki FAFU kwa ajili ya kusoma shahada ya uzamivu.
“Teknolojia ya Juncao ina manufaa kwa nchi zinazoendelea, hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo yanahitaji maendeleo,” amesema Aimable. "Mimi na mke wangu tutarudi nyumbani baada ya kumaliza masomo yetu nchini China na kupeleka teknolojia ya Juncao mahali tulikozaliwa ili kusaidia watu wa nchi yetu. Ninaamini watakuwa na maisha bora kwa kutumia teknolojia ya Juncao."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma