Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini na Senegal (2)
Wang Yi akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Senegal Bibi Yacine Fall. (Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China) |
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi jana Jumapili hapa Beijing amekutana kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Bw. Ronald Lamola na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Bibi Yacine Fall.
Katika mazungumzo hayo Bw. Wang Yi amesema China inaunga mkono kithabiti nchi za Afrika kulinda haki yake halali ya kujiendeleza, na iko tayari kushirikiana na Afrika kujenga nchi yenye ncha nyingi ambazo zina usawa na utaratibu, na kutafuta utandawazi wa uchumi wa dunia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika ya Kusini Bw. Lamola amesema, nchi yake inaunga mkono mapendekezo mfululizo ya China kwa Dunia, na kupenda kushirikiana na China kuhimiza kwa pamoja mshikamano na ushirikiano kati ya nchi za kusini.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Bibi Fall amesema wakati wa mkutano huo atafanya ziara ya kiserikali nchini China, ambayo pia ni ziara yake ya kwanza nje ya Afrika, na anatarajia kutumia fursa hii kuimarisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Senegal na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma