Lugha Nyingine
Meli ya Hospitali ya jeshi la?Majini la China “Peace Ark” yawasili Afrika Kusini kwa mara ya kwanza (3)
Meli ya hospitali ya kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ikiwasili kwenye bandari ya Cape Town, Afrika Kusini, tarehe 22, Agosti. (Xinhua/Liu Zhilei) |
Meli ya hospitali ya kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), “Peace Ark”, iliyo katika “Jukumu la Masikilizano 2024” imewasili katika Afrika Kusini Tarehe 22, Agosti na kuanza ziara yake kwa siku saba na kutoa huduma za matibabu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Meli ya hospitali “Peace Ark” kufanya ziara nchini Afrika Kusini.
Katika ziara yake hiyo, meli ya hospitali “Peace Ark” itatoa huduma za matibabu kwenye jukwaa lake kuu, na pia itapeleka timu za madaktari kwenye hospitali za huko kutoa huduma za matibabu kwa shirikiana na madaktari mbalimbali, kufanya mawasiliano ya kitaalamu, na kwenda katika Taasisi ya Confucius ya Matibabu ya jadi ya China katika Chuo Kikuu cha Western Cape kufanya shughuli maalum ya mawasiliano ya kitaaluma kuhusu Matibabu ya jadi ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma