Lugha Nyingine
Picha: Pazia la ulinzi wa usalama wa ikolojia Kaskazini Mashariki mwa China (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2024
Picha iliyopigwa kwa droni tarehe 18 Julai 2024 ikionyesha farasi wakiwa malishoni kwenye malisho ya Wulanmaodu, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Xinhua/Bei He) |
Ikiwa ni sehemu ya mashariki ya Mpango wa Misitu ya Ukanda wa Ulinzi wa Ikolojia wa Maeneo Matatu ya Kaskazini mwa China (yaani maeneo ya Kaskazini, Kaskazini Mashariki na Kaskazini Magharibi, unajulikana kama TSFP), ambao ni mradi mkubwa wa upandaji miti, eneo la kaskazini mashariki mwa China limeshuhudia uboreshaji endelevu wa mazingira ya kiikolojia. China ilipendekeza Juni 2023 kubadilisha mradi huo wa TSFP kuwa "Ukuta Mkuu wa Kijani" na kuwa Pazia la ulinzi wa usalama wa ikolojia kaskazini mwa China. Mpango huo ulioanzishwa mwaka 1978, unalenga kurejesha upya na kuyafanya kuwa ya kijani maeneo ya jangwa na maeneo yenye hali ya jangwa katika maeneo ya kaskazini, kaskazini magharibi, na kaskazini mashariki mwa China.?
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma