Lugha Nyingine
Watoto wa kimataifa wafanya mawasiliano?ya sanaa kaskazini mwa China
Watoto kutoka kundi la Sanaa la Uzbekistan wakitembelea maonyesho ya picha za kuchorwa ya Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Watoto la Tianjin Mwaka 2024 mjini Tianjin, Kaskazini mwa China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Zhao Zishuo)
TIANJIN - Tamasha la Sanaa la Kimataifa la Watoto la Tianjin Mwaka 2024 lenye kaulimbiu ya "Amani, Urafiki, Siku za Baadaye," limeanza siku ya Jumatatu jioni katika mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China, likivutia wasanii watoto zaidi ya 1,000 kutoka vikundi zaidi ya 50 vya sanaa vya nchi na maeneo 40.
Tamasha hilo la siku tano limepangwa kufanya shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maonyesho ya jukwaani, tamasha kubwa linalojumuisha watoto kutoka ndani na nje ya China, kupanda Ukuta Mkuu ya sehemu ya Tianjin na kufanya ziara za kuzunguka mji huo.
Liu Xinyi, mshiriki wa Kwaya ya Watoto ya Tianjin Cathay Future mwenye umri wa miaka 8, aliimba wimbo "Ode to Joy" kwenye hafla ya ufunguzi wa tamasha hilo. "Shuguli hii inaleta pamoja watoto kutoka duniani kote kama familia moja, yenye umoja, amani na furaha," amesema.
Ehab Gouda, Mkuu wa Kampuni ya Arabs Friendship Association, ameongoza kikundi cha sanaa cha watoto cha Misri kushiriki katika tamasha hilo la sanaa.
“Tamaduni za kucheza ngoma za China na Misri ni tofauti, lakini muunganisho wa hizi mbili unatoa mandhari ya kuvutia,” Gouda amesema
Li Ye, mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha Sanaa ya Ballet cha Oregon kutoka Marekani, ameongoza watoto 12 wa Marekani kushiriki tamasha hilo kwa mara ya kwanza.
"Sanaa haina mipaka. Natumai watoto wataona zaidi, kupata uzoefu zaidi, na kuhisi hisia maridadi katika utamaduni wa China, wakijichangamanisha wenyewe katika taswira ya wahusika wa ballet na kuwa mfano vielelezo wa mawasiliano ya utamaduni kati ya Mashariki na Magharibi katika siku zijazo." Li amesema.
Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Watoto la Tianjin limeshafanyika kwa awamu 10, likiwa na ushiriki wa watoto karibu 10,000 kutoka nchi na maeneo mbalimbali 100 katika kipindi cha miaka hiyo, kwa mujibu wa waandaaji.
Washiriki kutoka kwaya ya Romania wakiwa wanapiga picha kwenye Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Watoto la Tianjin Mwaka 2024 mjini Tianjin, Kaskazini mwa China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Zhao Zishuo)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma