Lugha Nyingine
Kaimu Rais wa Myanmar ahamishia madaraka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Utawala kutokana na hali ya kiafya
Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Januari 31, 2024 ikimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Serikali ya Myanmar (SAC) Jenerali Mwandamizi Min Aung Hlaing akiwa kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Ulinzi na Usalama la Myanmar huko Nay Pyi Taw, Myanmar. (Wizara ya Habari ya Myanmar / kupitia Xinhua)
YANGON - Madaraka ya Kaimu Rais wa Myanmar U Myint Swe yamekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Serikali ya Myanmar (SAC) Jenerali Mwandamizi Min Aung Hlaing, Redio na Televisheni ya Taifa ya Myanmar (MRTV) imeripoti habari hiyo siku ya Jumatatu ikisema kuwa taarifa ilikuwa tayari imeshatolewa kuwa Kaimu Rais U Myint Swe anapatiwa matibabu baada ya kuchukua likizo ya matibabu kutokana na hali yake ya kiafya.
Ofisi ya Kaimu Rais ilituma barua kwa Ofisi ya Mwenyekiti wa SAC ikisema kwamba madaraka ya Kaimu Rais yatakabidhiwa kwa Mwenyekiti wa SAC ili kutekeleza kazi za Baraza la Taifa la Ulinzi na Usalama la Myanmar (NDSC) kama itakavyohitajika, na kuchukua madaraka ya Kaimu Rais wakati akiwa hayupo, habari hiyo imesema.
Baada ya barua hii kutumwa, utiaji saini wa kukabidhi madaraka ulikamilika Jumatatu asubuhi ili kutekeleza kazi za NDSC, habari hiyo imesema.?
Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Januari 31, 2024 ikimuonyesha Kaimu Rais wa Myanmar U Myint Swe akiwa kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Ulinzi na Usalama la Myanmar huko Nay Pyi Taw, Myanmar. (Wizara ya Habari ya Myanmar / kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma