Lugha Nyingine
Maofisa wa kijeshi kutoka nchi 35 watembelea chuo kikuu cha jeshi la majini cha China mjini Dalian
Mshika usukani wa Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) akionyesha namna ya kushika usukani kwa maofisa wa kijeshi waliopanda meli ya kufanyia mazoezi, Julai 22, 2024. (Picha na Li Haotian/Xinhua)
DALIAN – Maofisa wa kijeshi kutoka ubalozi wa nchi 35 nchini China wametembelea Chuo kikuu cha Jeshi la Majini cha Dalian cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) katika Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China kuanzia Jumapili hadi Jumatatu ambapo ziara hiyo ilikuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano wa kijeshi wa kimataifa Mwaka 2024.
Wanadiplomasia hao wa kijeshi walioalikwa kwenye ziara hiyo wametoka katika ubalozi wa nchi mbalimbali nchini China zikiwemo Singapore, Australia na Hispania.
Kwenye ziara yao hiyo, maofisa hao wa kijeshi walishiriki kwenye hafla ya ufunguzi wa mashindano ya kimataifa ya boti za matanga, walitazama mafunzo kwenye darasa, na kupanda meli ya kufanyia mazoezi ili kujionea safari kwenye bahari. Pia walitembelea jumba la makumbusho ya historia la chuo hicho na kula chakula cha mchana na wanajeshi makadeti.
Kikijulikana kama "chimbuko la maofisa wanajeshi wa majini," Chuo kikuu cha Jeshi la Majini cha Dalian ni mojawapo ya vyuo vya kijeshi vilivyoanzishwa mapema zaidi baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuanzishwa Mwaka 1949. Kimetoa mafunzo kwa maofisa makamanda 60,000 wa Jeshi la Majini cha PLA, ikiwa ni pamoja na asilimia zaidi ya 80 ya manahodha wa meli zake.?
Maofisa wa kijeshi wakitazama mazoezi ya kijeshi wakiwa wamepanda meli ya kufanyia mazoezi ya Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Julai 22, 2024. (Picha na Li Haotian/Xinhua)
Maofisa wa kijeshi wakijipiga picha ya selfie wakiwa wamepanda meli ya kufanyia mazoezi ya Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Julai 22, 2024. (Picha na Li Haotian/Xinhua)
Maofisa wa kijeshi wakijionea safari kwenye bahari wakiwa wamepanda meli ya kufanyia mazoezi ya kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Julai 22, 2024. (Picha na Li Haotian/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma