Lugha Nyingine
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akutana na naibu spika wa Baraza la Wawakilishi la Japan
Zhao Leji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akikutana na Banri Kaieda, naibu spika wa Baraza la Wawakilishi la Japan, mjini Beijing, China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
BEIJING – Siku ya Jumatatu hapa Beijing, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China Zhao Leji amekutana na Banri Kaeda, naibu spika wa Baraza la Wawakilishi la Japan, ambapo Zhao amesema kuwa kudumisha na kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Japan kunaendana na maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizo mbili na kusaidia amani, utulivu na ustawi wa kikanda na Dunia nzima.
Amesema China ingependa kujiunga pamoja na Japan katika kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, kuendelea kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, na kufuata kanuni na maoni ya pamoja katika nyaraka nne za kisiasa kati ya China na Japan.
Zhao amesema, China pia ingependa kuzidisha mawasiliano na ushirikiano na Japan katika sekta mbalimbali, kusimamia na kushughulikia kwa kufaa masuala nyeti, kuhimiza maoni ya umma na mazingira ya kijamii yanayoweza kuleta hamasa za watu, na kusukuma mbele maendeleo mazuri na ya utulivu ya uhusiano wa pande mbili kwenye njia sahihi.
Bunge la Umma la China linapenda kudumisha mawasiliano ya kirafiki na Bunge la Japan na kuimarisha mawasiliano kwenye ngazi zote za mabunge, na linakaribisha wabunge wa Japan kutembelea China na kuijua hali yake halisi, ameongeza.
Kwa upande wake Kaieda amesema Baraza la Wawakilishi la Japan linapenda kuimarisha mawasiliano na Bunge la Umma la China, kutoa wito wa kuishi pamoja kwa amani, kupanua mawasiliano ya kiutamaduni, na kuongeza ushirikiano katika sekta za uchumi na utamaduni.
Zhao Leji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akikutana na Banri Kaieda, naibu spika wa Baraza la Wawakilishi la Japan, mjini Beijing, China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma