久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

China yaanza kikamilifu kazi ya nchi mwenyekiti wa zamu wa SCO

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 23, 2024

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema siku ya Jumatatu kuwa, China imeanza kazi kikamilifu ya kuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa Mwaka 2024 hadi 2025 baada ya mkutano wa kilele wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo huko Astana, Kazakhstan.

Msemaji Mao ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipotakiwa kueleza mpango wa China wa kutekeleza majukumu na wajibu wa nchi mwenyekiti wa zamu.

"Kufuatia mkutano wa kilele wa Astana mwezi Julai, China imekuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa SCO kwa 2024-2025, na itakuwa nchi mwenyeji wa mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo Mwaka 2025. China inatilia maanani sana kazi hiyo ya nchi mwenyekiti na imeanza kazi yake kikamilifu. "Mao amesema.

Akidhihirisha kuwa SCO imeendelezwa kuwa jumuiya ya ushirikiano wa kikanda wa pande zote ambayo inafikia eneo kubwa zaidi na idadi kubwa zaidi ya watu duniani, Mao amesema jumuiya hiyo inatoa mfano mzuri wa kuanzishwa kwa uhusiano wa kimataifa wa aina mpya, na kupata nadharia na uzoefu muhimu kwa ajili ya kutafuta njia za kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Katika muda wa miezi 12 ijayo, China itakuwa ikifanya ushirikiano wa karibu na washirika wa SCO katika sekta za siasa, usalama, uchumi na utamaduni na kuifanya jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai ioneshe vya kutosha kazi yake kama ngao ya usalama wa kikanda, daraja la ushirikiano, kiungo cha urafiki na nguvu ya kuelekea mambo mema katika kanda, msemaji huyo amesema.

China itatumia fursa nzuri ya kuwa nchi mwenyekiti wa zamu kujiunga na pande zote za SCO katika kuhimiza kujenga maskani ya pamoja yaliyo ya mshikamano na kuaminiana, amani na utulivu, ustawi na maendeleo, urafiki na ujirani mwema, haki na usawa, kuhimiza kujenga jumuiya ya ukaribu zaidi ya SCO yenye mustakabali wa pamoja na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kanda hiyo na kanda nyingine, msemaji huyo amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>