Lugha Nyingine
Paris "iko tayari" kwa Olimpiki, wasema waandaaji
Tony Estanguet (Kati) Rais wa Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Kituo Kikuu cha vyombo vya habari cha Paris 2024 Jijini Paris, Ufaransa, Julai 21, 2024. (Xinhua/Wang Dongzhen)
PARIS - Zikiwa zimebaki siku tano kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024 kufunguliwa, waandaaji wa michezo hiyo wamesema "wako tayari" kwa Michezo hiyo na wameahidi mto safi wa Seine.
"Tuko tayari tunapoelekea katika hatua ya mwisho," Tony Estanguet, Rais wa kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumapili. "Leo (jana Jumapili) tuko mahali ambapo tungekuwa tukiota ndoto kuwa miaka michache iliyopita."
Marekebisho ya mwisho yanafanywa katika kumbi na maeneo mbalimbali ya michezo mjini Paris, huku maelfu ya wanamichezo na maafisa wakiwasili mjini humo, na hali ya hewa ikiimarika kwa kiasi kikubwa.
Hasa, ubora wa maji ya Mto Seine, ambao utatumika kwa sherehe za ufunguzi, kwa mbio za marathon za kuogelea na triathlons, umeonekana kuboreshwa kwa kiasi kikubwa tangu mapema Julai, Estanguet amesema.
"Viashiria vyote vya Mto Seine ni vizuri katika hatua hii," Estatuet amesema.
Meya wa Paris Anne Hidalgo (Kulia) na Tony Estanguet wakiogelea kwenye Mto Seine siku chini ya 10 kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024, Julai 17, 2024. (Xinhua/Cao Can)
Mkuu huyo pia amezungumzia urithi wa kudumu wa kuboresha mazingira kupitia kuboresha ubora wa maji. "Tumetumia nguvu kubwa kwa hili katika miezi michache iliyopita, na vipimo vya hivi karibuni vinaonyesha kuwa kila kitu kiko kwenye kijani. Tunafuatilia kila kitu mara kadhaa kila siku," amesema.
"Kufikia 2025, tutabaki Mto Seine safi ambao watu wataweza kuogelea katika sehemu mbalimbali. Huo utakuwa urithi," Estanguet ameongeza.
Ukibeba jukumu muhimu katika sherehe za ufunguzi, Mto Seine utakaribisha wanamichezo 6,000 hadi 7,000 ndani ya mashua 85 na boti, ikiwa ni mara ya kwanza sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto kufanyika nje ya uwanja mkuu wa michezo.
Watazamaji hadi 300,000 walio na tiketi wanatarajiwa kutazama kutoka kwenye stendi na kingo za mto huo, huku wengine zaidi wapatao 200,000 wakitazama kutoka kwenye nyumba za makazi zilizo karibu.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma