Lugha Nyingine
Bibi Peng Liyuan ahudhuria shughuli ya Kambi ya Majira ya Joto ya Watoto ya China na Afrika
(Picha inatoka Xinhua)
Mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan amehudhuria na kuhutubia shughuli ya Kambi ya Majira ya Joto ya Watoto wa China na Afrika iliyofanyika kwenye maktaba ya Beijing, mjini Beijing mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika hotuba yake, Bibi Peng Liyuan amesema shughuli hiyo siyo tu ni sherehe ya watoto wa China na Afrika, bali pia imeonesha uhusiano wa karibu kati ya pande hizo mbili.
Amesema China ikiwa mshirika wa Afrika katika njia yake ya kujiendeleza siyo tu inafanya bidii kulinda ukuaji mzuri wa watoto wa China, bali pia inajikita kuchangia katika ukuaji wenye afya wa watoto wa Afrika.
Bibi Peng Liyuan amesisitiza kuwa, anatarajia watoto wa pande zote mbili za China na Afrika walioshiriki katika shughuli hiyo watakuwa warithi wa urafiki wa jadi kati ya China na Afrika na nguvu mpya wa kujenga Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma