久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Njia za anga zastawisha biashara ya nje katika mkoa wa milimani wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 22, 2024

Ndege ya mizigo ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Longdongbao huko Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Julai 13, 2024. (Xinhua)

Ndege ya mizigo ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Longdongbao huko Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Julai 13, 2024. (Xinhua)

GUIYANG - Kufuatia njia mpya ya ndege za mizigo inayounganisha Mji wa Guiyang katika Mkoa wa Guizhou wa China na Moscow, Russia kuanzishwa mapema mwezi huu, idadi ya njia za kimataifa za ndege za mizigo zilizounganishwa na mkoa huo wa Guizhou ulioko kusini-magharibi mwa China imefikia nne ambapo inaleta safari za ndege zenye ufanisi na rahisi zaidi kwa biashara.

Guizhou inajulikana kwa mandhari yake ya milima nchini China, ambayo inaleta changamoto kwa usafiri wa barabara na reli, na hivyo kuwa na haja ya kuendeleza usafiri wa anga.

Eneo la Kiuchumi la Shuanglong la Uwanja wa Ndege wa Guizhou, ambalo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guiyang Longdongbao ndiyo msingi wake mkuu, lilianzishwa Mwaka 2014. Mbali na njia hiyo mpya ya ndege za mizigo iliyofunguliwa, pia linaendesha njia tatu za ndege za mizigo zinazounganisha Mji wa Guiyang ambao ni mji mkuu wa mkoa huo na miji ya Kolkata na Delhi ya India, pamoja na Karachi nchini Pakistani.

Ikiwa imepakia bidhaa za samaki wa baharini kutoka Russia kama vile snow crabs, king crabs, na sea urchin, ndege ya mizigo ya IL-76 iliondoka Moscow kuelekea Guiyang Julai 13, na kurudi na bidhaa za China zenye uzito wa tani 40, hasa bidhaa za kielektroniki.

Njia hiyo kwa sasa inaboreshwa kulingana na soko. Lakini mwendeshaji wake amesema kama uendeshaji wa huduma hiyo ya uchukuzi utapokelewa vyema, safari za ndege za kwenda na kurudi zitakuwa za kila baada ya muda fulani kuanzia Septemba, jambo ambalo litapelekea kiwango cha biashara ya kuagiza na kuuza nje bidhaa cha kila mwaka cha Guizhou kufikia hadi karibu Yuan bilioni 3 (dola za Kimarekani karibu milioni 420.7), ikiwa na shehena ya bidhaa zenye uzito wa tani karibu 15,000.

Ilikuwa ikichukua saa 60 hadi 70 kusafirisha samaki wa baharini kutoka Russia hadi Guizhou kwa reli na bahari. Njia hiyo mpya ya anga inafupisha muda wa usafiri hadi saa 12 hadi 13, amesema Su Bowenhao anayefanya kazi Kampuni ya Usimamizi wa mnyororo wa usambazaji ya Guizhou First Catch.

Mizigo ikionekana kwenye ghala la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Longdongbao wa Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Julai 13, 2024. (Xinhua)

Mizigo ikionekana kwenye ghala la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Longdongbao wa Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Julai 13, 2024. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>