Lugha Nyingine
Reli ya mwendo kasi ya Rizhao-Lankao nchini China yaanza kufanya kazi kikamilifu (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2024
Wahudumu wa treni wakipiga picha katika Stesheni ya Reli ya Heze Mashariki mjini Heze, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Julai 18, 2024. (Xinhua/Guo Xulei) |
Sehemu ya reli ya mwendo kasi kutoka Mji wa Zhuangzhai katika Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China hadi Mji wa Lankao katika Mkoa wa Henan, Katikati mwa China imeanza kutumika siku ya Alhamisi, ikimaanisha kuanza kufanya kazi kikamilifu kwa reli nzima ya mwendo kasi ya Rizhao-Lankao yenye urefu wa kilomita 472.
Njia hiyo ya reli huanzia katika Stesheni ya Reli ya Rizhao Magharibi na kuishia katika Stesheni ya Reli ya Lankao Kusini, ikiunganisha miji kama vile Rizhao, Linyi, Jining, Heze, Shangqiu na Kaifeng, ambayo hupunguza sana muda wa kusafiri kati ya miji hiyo mikubwa katika mikoa hiyo ya Shandong na Henan.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma