Lugha Nyingine
Habari picha: Uchoraji wa picha ndani ya chupa huko Kunming, Mkoa wa Yunnan wa China (8)
Uchoraji wa picha ndani ya chupa ndogo ni aina ya sanaa ya jadi ya China. Hapo awali ilihusisha chupa ndogo za ugoro ambazo zilikuwa na picha zilizochorwa na Maandiko ya Kichina yaliyoandikwa ndani ya chupa.
Uchoraji huo wa picha unafanyika kwa kupenyeza brashi maalum kupitia mdomo wa chupa. Mchakato wa uchoraji, ambao hufanyika kwa kuijongesha brashi kabisa ndani ya chupa, ambapo mchoraji atatakiwa kuchora picha kwa usahihi kabisa.
Sun Hongyan, mchoraji mwenye umri wa miaka 49, amechora picha mbalimbali za mandhari za mazingira ya asili, mila na desturi za kikabila za Yunnan katika kazi zake za uchoraji picha ndani ya chupa ndogo, na hivyo amebuni uchoraji picha wa mtindo wa kipekee wa Yunnan wa sanaa hii.
Wakati wa kushikilia mbinu za jadi, wachoraji wamefanya ubunifu mpya, hivyo uchoraji picha ndani ya chupa unakaribishwa zaidi miongoni mwa vijana. "Tunainua uchoraji wa picha ndani ya chupa kwenye kiwango cha juu zaidi, tukichanganya ufundi huu wa kale na uzuri na sura mpya za zama tulizonazo," Sun amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma