Lugha Nyingine
Msimu wa Mavuno ya majira ya joto katika eneo la Hetao la Mongolia ya Ndani, China waanza rasmi (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 17, 2024
Kazi ya kuvuna ngano ikifanyika katika Kijiji cha Guangming cha Mji wa Bayannur wa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China. (Picha na Li Yunping/Xinhua) |
Siku ya Jumanne, Julai 16, hafla kwa ajili ya kuvuna ngano ngumu ya Hetao ya Mji wa Bayannur wa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China ilifanyika katika Kijiji cha Guangming cha mji huo, ikifungua msimu wa kuvuna ngano katika eneo zima la Hetao.
Mashamba ya ngano yenye ukubwa wa mu 450,000 (sawa na hekta 30,000) katika eneo la Hetao la Mongolia ya Ndani ambalo pia linafahamika kwa jina la “Ghala la Nafaka Kaskazini ya Ukuta Mkuu wa China”, yameingia kipindi cha mavuno.
Serikali ya eneo hilo imechukua fursa mwafaka ya hali nzuri ya hewa ya siku hizi na imeandaa mashine kubwa na za kati za kuvuna mazao kufanya kazi ya kuvuna ngano, ili kuhakikisha ngano inavunwa na kuhifadhiwa kwenye ghala.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma