<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>

    久久精品蜜芽国产亚洲av,国产成人观看免费全部完,1024综综合合久久AV,午夜国产成人精品,国产精品综合承认,国产高跟黑色丝袜在线

    Jumba la Makumbusho ya makaburi ya chini ya ardhi kwenye Njia ya kale ya Hariri lafunguliwa Xinjiang

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2024
    Jumba la Makumbusho ya makaburi ya chini ya ardhi kwenye Njia ya kale ya Hariri lafunguliwa Xinjiang
    Picha hii iliyopigwa tarehe 15 Julai 2024 ikionyesha mwonekano wa nje wa Jumba la Makumbusho ya eneo la mabaki ya Makaburi ya Kale ya Enzi za Wei na Jin katika Mji wa Kuqa, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China. (Xinhua/Ding Lei)

    URUMQI – Katika sehemu ya mita takriban nane chini ya mtaa wenye maduka mengi wa Mji wa Kuqa, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini-Magharibi mwa China, kuna makaburi ambayo yamefunikwa tuli chini ya ardhi kwa zaidi ya miaka 1,700. Hata hivyo, leo makaburi hayo, ambayo kihistoria yanaanzia kwenye Njia ya Kale ya Hariri, yamefukuliwa na kuoneshwa kwenye Jumba la Makumbusho la kipekee.

    Jumba hilo la makumbusho la chini ya ardhi la Makaburi ya Kale ya Enzi za Wei na Jin (220-420) limefunguliwa rasmi siku ya Jumatatu katika Wilaya ya Kuqa, sehemu ambayo hapo awali ilikuwa ya Dola ya Kale ya Qiuci.

    Dola ya Qiuci, ambayo ilianzishwa katika karne ya pili KK na ilidumu kwa zaidi ya miaka 1,000, ilikuwa mojawapo ya madola 36 katika “Maeneo ya Magharibi”. Maeneo hayo katika Enzi ya Han (206 BC-220 AD) yalikuwa maeneo ya magharibi ya Mpaka wa Yumen, yakiwa ni pamoja na Xinjiang ya sasa na sehemu za Asia ya Kati.

    Jumba hilo la makumbusho lenye mita za mraba 5,000 lilijengwa kwa ajili ya kulinda vyumba 15 vya matofali vya makaburi vilivyogunduliwa sehemu hiyo Mwaka 2007 wakati wa ujenzi wa barabara ya chini ya ardhi ya Youyi. Hilo lilikuwa moja ya magunduzi makubwa kumi mapya katika utafiti wa mambo ya kale ya China mwaka huo.

    Makaburi hayo yanafanana na makaburi ya mtindo wa Enzi ya Han yenye vyumba vya matofali yaliyogunduliwa katikati mwa China na kando ya Ukanda wa Hexi. Ukanda huo una umbali wa karibu kilomita 1,000 katika Mkoa wa Gansu, kaskazini-magharibi mwa China, na katika mkoa wa Gansu, kuna Maeneo Matano ya Mali ya Urithi wa Dunia ulioorodheshwa na UNESCO, na pia kuna mapango ya kale 53 ya mawe.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha

    久久精品蜜芽国产亚洲av
    <sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
    <noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>