Lugha Nyingine
Mazoezi ya pamoja ya vikosi vya wanajeshi wa majini vya China na Russia yaanza
GUANGZHOU - Manowari za vikosi vya wanajeshi wa majini vya China na Russia zimeng’oa nanga kutoka bandari ya jeshi la majini la China huko Zhanjiang, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, siku ya Jumatatu zikienda kufanya mazoezi ya kijeshi ya baharini ya siku tatu ambapo ikiwa ni sehemu muhimu ya mazoezi ya pamoja ya China na Urusi, mazoezi hayo yanahusu ulinzi wa kutia nanga, upelelezi wa pamoja na tahadhari ya mapema, utafutaji na uokoaji wa pamoja, na ulinzi wa pamoja wa anga na ulinzi wa makombora, wahusika wa upande wa majeshi wamesema.
Ufyatuaji wa risasi utafanywa ili kujaribu matokeo ya majadiliano na mabadilishano yaliyopita wakati wa kipindi cha upangaji. Zhang Xiaogang, msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China, alitangaza Ijumaa wiki iliyopita kwamba vikosi vya kijeshi vya China na Russia vilianza "Mazoezi ya Bahari ya Pamoja-2024" katika maji na anga karibu na Zhanjiang. Mazoezi hayo yamepangwa kuendelea hadi katikati ya Julai.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma