Lugha Nyingine
“Mazao mapya” kwenye paa la nyumba yaleta kipato wakati Jua linapomulika huko Gansu, China (2)
Paneli za kuzalisha umeme kwa Jua zikiwa kwenye mapaa ya nyumba za kijiji cha Xinji, Wilaya ya Hongsibao ya Mkoa wa Gansu wa China. (Picha na Kang Guoqing/Xinhua) |
Kuna “zao jipya” juu ya paa la nyumba ya Wang Jun, mwanakijiji wa Kijiji cha Youfang cha Wilaya ya Tongwei mkoani Gansu, China, ambalo linaweza kuvunwa chini ya mwanga wa Jua.
Katika siku za majira ya joto, baada ya kumaliza kazi ya kilimo ya shambani, Wang mwenye umri wa miaka 60 mara kwa mara huenda kwenye paa la nyumba yake na taratibu husafisha kwa makini “zao” lake lingine, ambalo ni vipande kumi vya paneli za kuzalisha umeme kwa nishati ya Jua.
"Tulifunga paneli za kuzalisha umeme kwa Jua kwenye nyumba yetu mwaka 2017 na umeme uliozalishwa nazo unauzwa kwenye gridi ya taifa, tukipata kipato cha Yuan zaidi ya 1,000 kila mwaka (takriban Dola za Marekani 137.7)" amesema Wang.
Umbali wa kilomita zaidi ya 300 kutoka hapa, katika Kijiji cha Xinji, Wilaya ya Hongsibao, safu za paneli za kuzalisha umeme kwa Jua kwenye paa ya nyumba ziko zinafyonza nishati ya mwanga na joto chini ya Jua kali linalochoma.
“Kila siku jua likimulika, tuna kipato thabiti.” Tian Shulin, naibu mkurugenzi wa Kijiji cha Xinji amesema, akiongeza kuwa, kufungwa kwa paneli hizo siyo tu kumesaidia kulipa ada za umeme kwa kupitia kipato chake, bali pia inakadiriwa kutaongeza kipato cha jumla cha kijiji hicho kwa karibu yuan 200,000 (sawa na Dola za Marekani 27540.6) kila mwaka.
Amesema kwa pesa hizo, wanakijiji wanaohitaji usaidizi wa haraka, kama vile wazee, wanaoumwa na wenye ulemavu, hawatakuwa na wasiwasi moyoni mwao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma