Lugha Nyingine
Upendo wa Mbrazili kwenye sanaa ya mapigano?na dawa za jadi za China (3)
Gabriel de Moraes Neto akifundisha wanafunzi Wushu huko Nanning, Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China, Julai 6, 2024. (Xinhua/Cao Yiming) |
Akiwa alizaliwa Mwaka 1978, Gabriel de Moraes Neto anatokea Rio de Janeiro, Brazil. Kwa sasa ni mkufunzi wa sanaa ya mapigano Wushu huko Nanning, Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China.
Akiwa alihamasishwa na Kung Fu ya Bruce Lee alipokuwa mdogo, Gabriel alianza kujenga shauku na sanaa ya mapigano ya China Wushu na alianza kupata mafunzo Mwaka 1999. Kadri uelewa wake wa Wushu na utamaduni wa jadi wa China ulipozidi, alijiita jina la "Mo Xiaolong," ambalo ni jina la Kichina la Bruce Lee, "Li Xiaolong."
Mwaka 2008, Gabriel aliwasili Chuo Kikuu cha Tiba ya Dawa za Jadi za China cha Beijing akiwa ni mwanafunzi wa mabadilishano na kujifunza acupuncture huku akifanya mazoezi ya Wushu. Kwake, Kung Fu inayojumuisha dawa za jadi za China (TCM) na uimarishaji wa mwili, inaonyesha haiba ya utamaduni wa Wachina.
Baada ya kumaliza masomo yake, Gabriel alirudi Brazil ambako alifungua shule maalumu kwa ajili ya mafunzo ya Kung Fu na kozi za acupuncture.
Mwaka 2011, Gabriel alitembelea tena China na kukutana na mchumba wake katika mji huo wa Nanning, ambaye alimuoa mwaka uliofuata nyumbani kwao Brazil. Mwaka 2016, Gabriel na mkewe walirudi Nanning na waliamua kukaa na kufanya kazi nchini China. Mara tu baada ya kurejea kwao, Gabriel alitambulishwa kwa mjuzi mbobezi wa Wushu wa eneo hilo Cai Rongkun na kuwa mkufunzi katika kilabu cha Wushu ya eneo hilo.
"Utamaduni wa jadi wa China unavutia sana. Nimejitolea kuendelea kujifunza," Gabriel amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma