Lugha Nyingine
Meli ya kijeshi ya Ufilipino iliyokwamishwa baharini kinyume cha sheria yaharibu mfumo wa ikolojia katika Kisiwa cha Ren'ai Jiao
Picha hii iliyopigwa tarehe 8 Julai 2024 kwenye hafla iliyofanyika Beijing ya kutolewa kwa matoleo ya Kichina na Kiingereza ya Ripoti ya Uchunguzi kuhusu Uharibifu wa Mfumo wa Ikolojia wa Miamba ya Matumbawe uliosababishwa na Meli ya Kijeshi ya Ufilipino Iliyokwamishwa Baharini kinyume cha sheria kwenye Kisiwa cha Ren'ai Jiao. (Xinhua/Li Xin)
BEIJING - Meli ya kijeshi ya Ufilipino ambayo imekwamishwa baharini kinyume cha sheria kwenye mteremko wa rasi ya Kisiwa cha Ren'ai Jiao tangu Mwaka 1999 imeharibu sana anuwai, uthabiti na uendelevu wa mfumo wa ikolojia ya miamba ya matumbawe katika eneo hilo, imesema Ripoti ya Uchunguzi juu ya Uharibifu wa Mfumo wa Ikolojia ya Miamba ya Matumbawe uliosababishwa na meli hiyo.
Uchunguzi huo umefanywa na Kituo cha Ikolojia ya Bahari ya Kusini na Idara ya Utafiti wa Maendeleo ya Bahari ya Kusini ya Wizara ya Maliasili ya China pamoja na taasisi nyingine na unatokana na uchunguzi wa kisayansi uliofanywa juu ya mfumo wa ikolojia wa miamba ya matumbawe kwenye kisiwa hicho na maeneo yake ya karibu ya bahari mwezi Aprili mwaka huu.
Uchunguzi huo umegundua kuwa mchakato wa kukwamisha meli hiyo baharini umesababisha uharibifu mkubwa kwa mfumo wa ikolojia wa miamba ya matumbawe, na hali yake ya kukwamishwa kwa muda mrefu imezuia sana ukuaji na urejeshaji wa matumbawe katika eneo jirani.
Umande ya metali nzito uliosababishwa na kutu ya meli hiyo, pamoja na utupaji wa taka za majumbani na maji taka unaofanywa na wafanyakazi walioko ndani ya meli hiyo, vimesababisha madhara ya kudumu kwa afya ya matumbawe, ripoti hiyo imesema.
Afya ya mfumo wa ikolojia ya miamba ya matumbawe pia imeathiriwa sana na taka za uvuvi zilizotupwa na wafanyakazi hao na boti za uvuvi za Ufilipino, imesema ripoti hiyo.
Uchunguzi huo umefanywa kwa njia ya kuhisi kwa mbali kwa kutumia satelaiti na kufanya uchunguzi kwenye eneo husika, ripoti hiyo imeeleza.
Uchunguzi huo umefanywa katika vituo 18 vya uchunguzi kando ya ukingo wa jukwaa la miamba, ukihusisha tathmini ya vigezo 75 katika makundi manne, ambayo ni jumuiya za matumbawe, viumbe, makazi na shughuli za binadamu kwenye miamba, imesema ripoti hiyo.
China ina mamlaka ya nchi isiyopingika kwenye Visiwa vya Nansha (Nansha Qundao) na eneo la bahari lililoko karibu navyo, ikiwa ni pamoja na Ren'ai Jiao, imesema ripoti hiyo.
Meli hiyo ya kijeshi ya Ufilipino ilikwamishwa baharini kinyume cha sheria kwenye mteremko wa rasi ya Ren'ai Jiao Mwaka 1999. Serikali ya China mara moja iliwasilisha upingaji rasmi na kutaka meli hiyo kuondolewa mara moja. Upande wa Ufilipino umekuwa ukiahidi mara kwa mara kuondoa meli hiyo, lakini hadi leo, ahadi hiyo bado haijatekelezwa.
Picha hii ikionyesha boya likiwa kaskazini mwa meli ya kijeshi ya Ufilipino iliyokwamishwa baharini kinyume cha sheria kwenye maji yanayozunguka Kisiwa cha Ren'ai Jiao cha China. (Picha inatoka Kituo cha Ikolojia ya Bahari ya Kusini na Idara ya Utafiti wa Maendeleo ya Bahari ya Kusini ya Wizara ya Maliasili ya China/Xinhua)
Picha hii iliyopigwa tarehe 8 Julai 2024 ikionyesha hafla iliyofanyika Beijing ya kutolewa kwa Ripoti ya Uchunguzi kuhusu Uharibifu wa Mfumo wa Ikolojia wa Miamba ya Matumbawe uliosababishwa na Meli ya Kijeshi ya Ufilipino Iliyokwamishwa Baharini kinyume cha sheria kwenye Kisiwa cha Ren'ai Jiao. (Xinhua/Li Xin)
Picha hii ikionyesha nyuzi za uvuvi chini ya bahari kwenye eneo la Kisiwa cha Ren'ai Jiao cha China. (Picha inatoka Kituo cha Ikolojia ya Bahari ya Kusini na Idara ya Utafiti wa Maendeleo ya Bahari ya Kusini ya Wizara ya Maliasili ya China/Xinhua)
Picha hii ikionyesha vyavu za uvuvi chini ya bahari kwenye eneo la Kisiwa cha Ren'ai Jiao cha China. (Picha inatoka Kituo cha Ikolojia ya Bahari ya Kusini na Idara ya Utafiti wa Maendeleo ya Bahari ya Kusini ya Wizara ya Maliasili ya China/Xinhua)
Picha hii ikionyesha matumbawe yaliyokufa chini ya meli ya kijeshi ya Ufilipino iliyokwamishwa baharini kinyume cha sheria kwenye eneo la Kisiwa cha Ren'ai Jiao cha China (Picha inatoka Kituo cha Ikolojia ya Bahari ya Kusini na Idara ya Utafiti wa Maendeleo ya Bahari ya Kusini ya Wizara ya Maliasili ya China/Xinhua)
Picha hii iliyopigwa tarehe 8 Julai 2024 ikionyesha hafla iliyofanyika Beijing ya kutolewa kwa Ripoti ya Uchunguzi kuhusu Uharibifu wa Mfumo wa Ikolojia wa Miamba ya Matumbawe uliosababishwa na Meli ya Kijeshi ya Ufilipino Iliyokwamishwa Baharini kinyume cha sheria kwenye Kisiwa cha Ren'ai Jiao. (Xinhua/Li Xin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma