Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na Rais Lukashenko wa Belarus
Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Alexander Lukashenko wa Belarus. (Picha na Pang Xinglei/Xinhua)
Mchana wa tarehe 4, Julai kwa saa za Kazakhstan, rais Xi Jinping wa China alikutana na rais Alexander Lukashenko wa Belarus wakati alipohudhuria kwenye Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana, Kazakhstan.
Xi alipongeza Belarus kuwa nchi mwanachama rasmi wa SCO. Xi alisema kuwa, rais Lukashenko alifanya ziara mara mbili nchini China mwaka 2023, ambapo tulipanga pamoja mpango mpya wa maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote wa siku zote kati ya China na Belarus. Tokea mwanzo wa mwaka huu, mawasiliano ya karibu yamedumishwa kwenye ngazi mbalimbali kati ya China na Belarus, na maoni yetu ya pamoja yametekelezwa vizuri. Inaaminika kuwa kupitia juhudi za pamoja za pande zetu mbili, ni hakika uhusiano wa China na Belarus utadumisha hali nzuri na kusonga mbele kwa hatua kubwa.
Lukashenko alisema, anashukuru upande wa China kuunga mkono Belarus kujiunga rasmi na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, na anapongeza China kuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa jumuiya hiyo. Upande wa Belarus unaunga mkono Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia, na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia yaliyotolewa na rais Xi Jinping, na unaunga mkono maoni sita ya pamoja yaliyotolewa na China na Brazil kuhusu kutatua msukosuko wa Ukraine kwa kupitia njia ya kisiasa. Anatarajia ushirikiano wa pande mbili au pande nyingi kati ya Belarus na China utakuwa wa karibu zaidi.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Alexander Lukashenko wa Belarus. (Picha na Pang Xinglei/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma