Lugha Nyingine
Viwanda 25 kutoka China vyashiriki kwenye maonesho ya Sabasaba Dar es salaam
Viwanda 25 kutoka nchini China vitashiriki maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba, kwa lengo la kuonyesha bidhaa wanazozalisha, kuwasiliana na wafanyabiashara wa Tanzania na kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kuwavutia wawekezaji Tanzania.
Miongoni mwa viwanda vilivyokuja ni pamoja na vya nguo, vifaa vya majumbani, simu, nishati ya jua, viatu, mitambo, vinywaji, Jenereta, magari, vyakula, na bidhaa za urembo, ambapo watatumia maonesho hayo kuuza na kuonesha bidhaa zao.
Mwandalizi wa maonesho hayo amesema baada ya kuona changamoto wanazopitia Wafanyabiashara wa Tanzania, vijana wa Tanzania waliosoma China waliona kuna haja ya kuwasaidia wafanyabiashara kwa kuwaunganisha na makampuni ya China kufanya biashara na kupata mizigo yao kwa wakati.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma