久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Simulizi za Njia ya Hariri za Rais Xi Jinping: Zama Mpya Inaanza nchini Kazakhstan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2024

Astana, Mji Mkuu wa Kazakhstan, ni mahali pa kuzaliwa kwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ikiashiria kuanza kwa zama mpya ya Njia ya Hariri.

"Ili kujenga uhusiano wa karibu zaidi wa kiuchumi, kuzidisha ushirikiano na kupanua nafasi ya maendeleo katika eneo la Eurasia, tunapaswa kuchukua njia ya kibunifu na kwa pamoja kujenga 'ukanda wa kiuchumi kando ya Njia ya Hariri'. Hili litakuwa jukumu kubwa la kunufaisha watu wa nchi zote kando ya njia hiyo," alisema Rais Xi Jinping katika hotuba yake yenye kichwa cha "Kuhamasisha Urafiki kati ya Watu na Kujenga Mustakabali Bora Pamoja" huko Astana tarehe 7, Septemba, 2013, ambako alipendekeza kwa mara ya kwanza pendekezo la Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri.

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa nchi tano za Asia ya Kati wakipanda miti sita ya mkomamanga ambayo inawakilisha mshikamano na ushirikiano wa karibu kati ya China na Asia ya Kati baada ya Mkutano wa kwanza wa Viongozi wa China na Asia ya Kati uliofanyika huko Xi’an, China, Mei 19, 2023. (Picha: Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa nchi tano za Asia ya Kati wakipanda miti sita ya mkomamanga ambayo inawakilisha mshikamano na ushirikiano wa karibu kati ya China na Asia ya Kati baada ya Mkutano wa kwanza wa Viongozi wa China na Asia ya Kati uliofanyika huko Xi’an, China, Mei 19, 2023. (Picha: Xinhua)

"Hotuba ya Rais Xi imekuwa sehemu ya historia tukufu ya chuo kikuu chetu," amesema Aisulu Tuktubayeva, ambaye alishiriki tukio hilo mwaka 2013. Amesema kwamba pendekezo la Rais Xi la Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri kwa kiasi kikubwa lilihamasisha kila mmoja, likiwafanya waamini kwamba "fursa mpya ya maendeleo kwa Kazakhstan imefika."

Akizungumzia juu ya kuboresha mawasiliano ya sera, muunganiko wa barabara, uwezeshaji wa biashara, mzunguko wa fedha na uhusiano kati ya watu, Rais Xi alisema, "tunaweza kuanza na kazi katika baadhi ya maeneo na kuyaunganisha siku hadi siku hadi kufikia kanda nzima."

Njia ya Kale ya Hariri haikuwa tu njia ya biashara bali pia njia ya urafiki. Mabadilishano ya kirafiki kati ya China na nchi nyingine kando ya njia hii yameunda moyo wa Njia ya Hariri wa amani na ushirikiano, uwazi na ujumuishaji, kufunzana na kunufaishana.

Hivi leo, Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limekita mizizi katika Kazakhstan, likizaa matunda ya mafanikio.

Kwenye eneo la mafunzo la Karakana ya Luban katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kazakhstan ya Mashariki (EKTU), wanafunzi wanafuata maelekezo ya walimu wao, wakijifunza uendeshaji na kanuni za vifaa vya matengenezo ya magari na kufanya masomo kwa vitendo. Karakana hiyo ya Luban, iliyojengwa kwa pamoja na Taasisi ya Ufundi ya Tianjin ya China na EKTU, ilianzishwa kwa ajili ya kukidhi hitaji la Kazakhstan la ufundi wa kitaaluma.

Kama usemi wa Kazakhstan unavyosema: "palipo na mshikamano, furaha hufuata." Katika miaka ya hivi karibuni, China na Kazakhstan zimeshikilia kanuni za kupanga pamoja, kujenga pamoja na kunufaika pamoja, zikitekeleza kwa mafanikio miradi kadhaa muhimu ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, ikinufaisha kwa upana watu wa nchi zote mbili.

Mnara wa Baiterek, pia ukijulikana kama “Mti wa Maisha” uliopo    matembezi ya kati ya Astana, Kazakhstan. (Picha na Cao Shulin/People’s Daily)

Mnara wa Baiterek, pia ukijulikana kama “Mti wa Maisha” uliopo matembezi ya kati ya Astana, Kazakhstan. (Picha na Cao Shulin/People’s Daily)

Katika miaka ya hivi karibuni, viongozi wa nchi hizo mbili wameweka kwa pamoja lengo la kujenga jumuiya ya China na Kazakhstan yenye mustakabali wa pamoja, kuweka kiwango kipya cha maendeleo ya uhusiano wa pande mbili, kutoa msukumo mpya na kufungua matarajio mapya.

Rais wa Kazakhstan, Tokayev, alisema kwamba Kazakhstan ni mshirika mzuri ambaye China anaweza kumwamini wakati wote. Alisema, Kazakhstan inaunga mkono kikamilifu Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia yaliyotolewa na Rais Xi, na iko tayari kudumisha mabadilishano ya ngazi ya juu na China, kuimarisha kushabihiana kimkakati kwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na ujenzi wa Ukanda wa Kati, kuhimiza maendeleo makubwa katika ushirikiano wa kiuchumi, kibiashara na kiutamaduni wa pande mbili, na kushiriki katika ushirikiano wa karibu zaidi na wenye ufanisi zaidi na China juu ya masuala ya kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>