Lugha Nyingine
Uwanja wa kwanza wa urushaji roketi wa kibiashara nchini China wajiandaa kwa uendeshaji rasmi (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2024
Picha hii iliyopigwa tarehe 30, Juni, 2024 ikionesha uwanja wa urushaji roketi wa kibiashara wa Hainan, Kusini ya China ukifanya mazoezi ya kurusha roketi. (Picha na Pu Xiaoxu/Xinhua) |
Tarehe 30, Juni, Uwanja wa Urushaji Roketi wa kibiashara wa Hainan ulioko Mji wa Usafiri kwenye Anga ya Juu wa kimataifa wa Wenchang, ambao ni eneo muhimu la Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, China, ulifanya mazoezi ya pamoja kwa vituo viwili vya urushaji roketi, ili kujiandaa kwa kazi ya kwanza ya kurusha roketi kwenye anga ya juu inayokaribia.
Huo ni uwanja wa kwanza wa urushaji roketi wa kibishara nchini China, ukijengwa na Kampuni ya Urushaji Roketi wa Biasharsa ya Kimataifa ya Hainan. Uwanja huo unalenga kujenga uwanja bora wa kimataifa wa kurusha roketi kwenye anga ya juu unaoendeshwa kwa kufuata kanuni za soko, na kuendelea kuongeza uwezo wa China wa kurusha roketi ya uchukuzi ya kibishara.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma