Lugha Nyingine
Chombo cha Chang'e-6 cha China chaleta duniani sampuli za kwanza kutoka upande wa mbali wa Mwezi (6)
Picha iliyopigwa Juni 25, 2025 ikionyesha eneo la kupokea na kuchukua chombo cha kurudia duniani ya chombo cha uchunguzi wa mwezi cha Chang'e-6 huko Siziwang Banner, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Bei He) |
BEIJING – Chombo cha kurudia duniani cha utafiti wa Mwezi cha Chang'e-6 cha China kimetua duniani siku ya Jumanne, na kuleta duniani sampuli za kwanza zilizokusanywa kutoka upande wa mbali wa Mwezi, ikionyesha mafanikio mengine ya ajabu katika juhudi za China za utafiti kwenye anga ya juu.
Idara ya kitaifa ya Anga ya Juu ya China imesema, chombo hicho kimetua kwa usahihi kabisa katika eneo lililokuwa limepangwa huko Siziwang Banner, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China saa 8:07 mchana (Saa za Beijing), kikifanya kazi kwa kawaida, na jukumu la chombo hicho limefanikiwa kutekelezwa.
Chombo hicho kitawasilishwa kwa ndege hadi Beijing ili kufunguliwa, na sampuli zilizopatikana kwenye Mwezi zitahamishiwa kwa timu ya wanasayansi ili kuhifadhiwa, kufanyiwa uchambuzi na utafiti, imesema CNSA.
Jukumu la chombo cha Chang'e-6 ni moja ya majukumu mazito na yenye changamano katika juhudi za China za kufanya utafiti kwenye anga ya juu hadi sasa. Kikiwa kinaundwa na chombo cha obita, chombo cha kurudia duniani, chombo cha kutua kwenye Mwezi na chombo cha kupandisha juu, kilirushwa kwenda Mwezi Mei 3 mwaka huu.
Juni 4, chombo cha kutembea kwenye Mwezi kiliondoka na sampuli hizo, na kuingia kwenye obiti ya Mwezi. Juni 6, kilikamilisha minyumbuliko na kutia nanga kwenye muunganisho wa obita na chombo cha kurudia duniani na kuhamisha sampuli kwenye chombo cha kurudia duniani. Kisha chombo hicho cha kutembea kwenye mwezi kilijitenga na muunganisho huo na kutua kwenye njia iliyo chini ya udhibiti wa kituo duniani ili kuepuka kuwa takataka kwenye anga ya juu.
"Jukumu la Chang'e-6 linawakilisha hatua muhimu katika historia ya utafiti wa mwezi wa binadamu, na litachangia uelewa mpana zaidi wa mwenendo na mabadiliko ya Mwezi," amesema Yang Wei, mtafiti wa Taasisi ya Jiolojia na Jiofizikia katika Taasisi kuu ya Sayansi ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma