Lugha Nyingine
China iko tayari kusukuma uhusiano na Poland hadi ngazi ya juu: Rais Xi
Rais wa China Xi Jinping akipeana mkono na Rais wa Poland Andrzej Duda, ambaye yuko Beijing kufanya ziara ya kiserikali nchini China, Juni 24, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei) |
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatatu alipokuwa na mazungumzo mjini Beijing na Rais wa Poland Andrzej Duda, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China ameahidi nia ya China kushirikiana na Poland katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi ya juu na kuleta utulivu na uhakika zaidi katika dunia yenye misukosuko.
Akisema kuwa, Poland ni moja ya nchi za kwanza kuitambua Jamhuri ya Watu wa China, Rais Xi amesema uhusiano wa pande mbili umedumisha maendeleo thabiti tangu nchi hizo mbili zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 75 iliyopita.
Tangu uhusiano kati ya China na Poland umeinuliwa kuwa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote miaka minane iliyopita, mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali umepanuka na kuendelezwa kwa kina, na kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.
Akibainisha kuwa mabadiliko makubwa yanatokea duniani kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa, Rais Xi amesema China ingependa kujiunga pamoja na Poland katika kushikilia Kanuni tano za Kuishi Pamoja kwa Amani, kushikilia nia ya awali ya wakati wa kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, kuendeleza urafiki wa jadi, kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi ya juu, na kuingiza utulivu na uhakika zaidi katika Dunia yenye misukosuko.
China imeamua kutekeleza sera ya siku 15 ya kuingia na kuishi China bila visa kwa raia wa Poland, Rais Xi amesema, huku akiongeza kuwa pande zote mbili zinapaswa kuhimiza kwa nguvu mawasiliano katika mambo ya utamaduni, kati ya vijana, sekta ya taaluma na kati ya vyombo vya habari.
Ameongeza kuwa China ingependa kushirikiana na Poland na nchi nyingine katika kuhimiza maendeleo endelevu ya mfumo wa ushirikiano kati ya China na Ulaya ya Kati na Mashariki, na kuendeleza maendeleo mazuri na tulivu ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
Kwa upande wake Duda amesema ziara ya Rais Xi nchini Poland mwaka 2016 ilikuwa hatua muhimu katika maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.
Pendekezo la Rais Xi la Ukanda Mmoja, Njia Moja linawakilisha fursa kubwa za maendeleo kwa Poland, na ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umechochea sana ujenzi wa miundombinu na maendeleo ya kiuchumi ya Poland, amesema.
Poland inathamini sana kanuni zinazofuatwa na China katika masuala ya kimataifa na mchango wake kwa amani na maendeleo ya dunia, Duda amesema, huku akisisitiza kuwa Poland inashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma