Lugha Nyingine
Wekeza katika Mkoa?wa Xinjiang, China | Ukuaji wa Nyanya ndogo Wategemea data kubwa
Mafungu ya nyanya ndogo kwenye Bustani ya Kilimo cha Teknolojia za Kisasa ya Runtai yakiwa tayari na rangi nyekundu. (Picha na Obulai/ People's Daily Online) |
"Banda hili la kioo la kilimo cha kisasa lenye hali ya hewa ya majira ya mchipuo mwaka mzima limejaa teknolojia ya hali ya juu." Tang Yue, mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya Kilimo ya Runtai katika Mji wa Kokdala, Kitengo cha Nne cha Kikosi cha Uzalishaji na Ujenzi cha Mkoa wa Xinjiang, China amesema huku akiongeza kuwa nyanya katika banda la Bustani ya Kilimo cha Teknolojia za Kisasa ya Runtai zote zilipandwa na kukuzwa kwa kilimo kisichotumia udongo, na vifaa mbalimbali vya kuhisi vimefungwa ndani ya banda hilo.
Kupitia teknolojia za kidijitali za uzalishaji, kutumia ipasavyo nguvu bora maalum ya kijiografia mkoani Xinjiang, kama vile muda mrefu wa mchana na tofauti kubwa za halijoto kati ya mchana na usiku, nyanya za banda hilo zinakua vizuri, na kuonekana kuwa mafungu mengi ya nyanya zenye rangi nyekundu angavu, umbo kamili la sikio la mfupa wa samaki, na ya ladha nzuri yenye uwiano sawa wa chachu na utamu.
"Tunatumia teknolojia za kisasa za kilimo za kizazi cha tatu za Uholanzi. Ikilinganishwa na upandaji wa jadi wa shamba, njia ya upandaji kwenye bustani ina nguvu bora dhahiri, huku ikiwa na uzalishaji mazao wa kila mwaka zaidi ya mara 5-6, na matumizi ya maji ya umwagiliaji ni 1/20 tu ya kiasi cha maji kinachotumika katika kilimo cha jadi, na bila kutoa uchafuzi zaidi kwa mazingira." Tang Yue amesema, akiongeza kuwa nyanya hizi ndogo katika mafungu zimepewa maana zaidi ya teknolojia ya kilimo.
Kwa sasa, mazao yanayopandwa kwenye bustani hiyo hasa ni nyanya hizo ndogo zilizo katika mafungu na cherries Na.8 za Russia. "Mavuno ya nyanya ndogo hizo ni kilo 22 hadi 25 kwa kila mita ya mraba, na mavuno kwa kila mu yanaweza kufikia tani 16. Mauzo ya kila mwaka yanatarajiwa kufikia yuan milioni 40. Eneo lenye ukubwa wa Mu 20 za cherries Na.8 za Russia linaweza kufikia mavuno ya Kilo 1,500 kwa kila mu baada ya mavuno mengi, na faida ni kubwa sana." Tang Yue amesema huku akionesha imani kubwa sana kuhusu matarajio ya "fedha" ya bustani hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma