Lugha Nyingine
Maisha ya michezo karibu na?ukuta wa Mji wa Kale mjini Xi'an, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2024
Picha iliyopigwa Juni 12, 2024 ikionyesha wakaazi wakifanya mazoezi ya Wushu karibu na ukuta wa mji wa kale mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha na Niu Gang/Xinhua) |
Mji wa Xi'an, katika Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China, ambao ni mji wenye historia ya miaka zaidi ya 3,100, ulikuwa ukitumika kama mji mkuu wa enzi 13 za China ya kale. Pia ulikuwepo sanamu za wapiganaji mashujaa maarufu duniani wa Terracotta walioundwa wakati wa Enzi ya Qin (221-207 KK).
Mji huo unajivunia kuta za mji wa kale zilizohifadhiwa vizuri zilizokuwa zikitumiwa kama ngome za ulinzi wa kijeshi. Kuta za mji huo wa kale ambazo zinajulikana zaidi zilijengwa kutoka Mwaka 1370 hadi 1378 wakati wa Enzi ya Ming (1368-1644) zikiwa na jumla ya urefu wa kilomita 13.7.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma