Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akagua Mkoa wa Ningxia Kaskazini Magharibi mwa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2024
YINCHUAN - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amekagua Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia Kaskazini Magharibi mwa China siku ya Jumatano ambapo alitembelea jumuiya ya makazi katika mji wa Yinchuan, ambao ni mji mkuu wa mkoa huo, na kufahamishwa kuhusu namna matawi ya Chama mashinani yanavyotekeleza majukumu yao.
Rais Xi Pia amefahamishwa kuhusu kazi ya jumuiya katika kuboresha huduma kwa wakazi na kuwezesha mawasiliano na mwingiliano kati ya watu wa makabila tofauti.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma