Lugha Nyingine
Kuwekeza Xinjiang, China: Maisha ya wafugaji wa ng’ombe
Picha ikionesha kituo cha kisasa cha kuzaliana mifugo mjini Cocodala, Xinjiang, China. (Picha na Li Xinyang/People’s Daily Online) |
Mnamo mwezi Juni, katika kituo cha kisasa cha kuzaliana ng'ombe kilichoko Cocodala, Mkoa wa Xinjiang wa China, ng'ombe wenye afya walikuwa wakikula malisho na kutembea taratibu.
“Hili ni shamba letu la kuzaliana ng'ombe bora, ambalo linakuza ng'ombe zaidi ya 10,000. Tuna vituo zaidi ya kumi vya kuzalisha kama hiki, na kiwango chao cha kuzaliana kinashika nafasi ya mbele nchini China,” amesema Li Jiongchun, mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kilimo na Ufugaji ya Xinjiang Chuangjin.
Hivi sasa Xinjiang inafanya kila jitihada kuhimiza ujenzi wa “makundi manane ya viwanda”, moja kati ya makundi hayo ni viwanda vya bidhaa bora za mifugo.
Tangu ianzishwe, Kampuni ya Chuangjin imewekeza jumla ya Yuan bilioni 2, vifaa vyake vya kuzalisha mifugo vinachukua eneo lenye ukubwa wa zaidi ya mu 4,000 (takriban hekta 267). Mwaka jana, ng'ombe zaidi ya 30,000 walipelekwa kutoka kituo cha kampuni hiyo hadi sehemu mbalimbali nchini China, na kuwa chakula kitamu cha mezani.
Li amesema, licha ya kuzalisha ng'ombe bora na kukuza ng'ombe wa nyama, kampuni hiyo pia imejenga kiwanda cha malisho, kiwanda cha mbolea ya samadi, kiwanda cha kusindika bidhaa za maziwa, kiwanda cha uchinjaji ng'ombe na usindikaji chakula na kiwanda cha kuzalisha mashine za kilimo na ufugaji, ambavyo vimeunda mnyororo kamili.
“Tunasaini mikataba ya oda za kupanda malisho mbalimbali kwenye mashamba yenye ukubwa wa karibu mu laki moja (takriban hekta 6667) kila mwaka, ambayo imesababisha wakulima wengi wa maeneo ya karibu kuongeza kipato chao,” amesema Li Jiongchun.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma