Lugha Nyingine
Mkoa wa Guangxi, China watafuta fursa za ufunguaji mlango, ukuzaji wa shughuli za kibahari na kuhimiza maendeleo ya sifa bora (6)
Picha ikionyesha kituo cha kontena cha reli huko Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China Zhuang, Mei 20, 2024. (Xinhua/Cao Yiming) |
Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China umekuwa ukitafuta fursa za ufunguaji mlango na ukuzaji wa shughuli za kibahari ili kuhimiza maendeleo ya sifa bora kupata mafanikio makubwa zaidi.
Mkoa wa Guangxi ni lango muhimu la China la kufungua mlango kwa Dunia na kufanya ushirikiano na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN), na ni kituo muhimu kwenye Ukanda Mpya wa Kimataifa wa Biashara ya Nchi Kavu na Baharini.
Ukiwa ulianzishwa Mwaka 2017, Ukanda Mpya wa Kimataifa wa Biashara ya Nchi Kavu na Baharini ni njia ya biashara na usambazaji wa bidhaa iliyojengwa kwa pamoja na mikoa mbalimbali ya magharibi mwa China na nchi wanachama wa ASEAN, ambayo imewezesha sana mageuzi ya kiuchumi ya Guangxi na kuendeleza ukuaji wake wa uchumi.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma