Lugha Nyingine
Maonyesho ya biashara ya utalii yatarajia kuendeleza zaidi soko la China (2)
Watu wakitembelea banda la Italia kwenye maonyesho ya ITB China 2024 mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Mei 27, 2024. (Xinhua/Chen Aiping) |
SHANGHAI – Maonyesho ya ITB China 2024 ambayo ni maonyesho makubwa ya kati ya kampuni za biashara ya utalii ambayo yanajikita katika kusaidia waendeshaji biashara ya utalii na wataalamu wa sekta hiyo kuendeleza zaidi shughuli zao kwenye soko la utalii la China yamefunguliwa Jumatatu mjini Shanghai.
Yakiwa yamepangwa kufanyika Mei 27 hadi 29, maonyesho hayo yameshirikisha kampuni zaidi ya 600 za kuonesha bidhaa na huduma kutoka nchi na maeneo zaidi ya 80.
Maonyesho hayo ya mwaka yana kaulimbiu ya "Jitahidi katika Mageuzi, Fikia Viwango Vipya. Tuko Pamoja," inayoangazia umuhimu wa kulingana na hali halisi na kufanya uvumbuzi katika shighuli za utalii, ikiwa ni pamoja na uwezo mkubwa wa kifursa, ambao haujatumiwa ipasavyo wa soko la utalii la China.
Maonyesho ya ITB China 2024 yamepanuka kwa asilimia 60 kutoka mwaka jana na yanajumuisha mihadhara mbalimbali, mijadala ya jopo na midahalo ili kuongeza ushirikiano na kuungana mkono.
"Tangu Mwaka 2023, soko la utalii la China limeendelea kwa mwelekeo mzuri, na kwenye matokeo mazuri ya kuboreshwa kwa sera za visa na kuongezeka kwa usafiri wa ndege, soko la utalii la China linaonyesha dalili kubwa za ukuaji mwanzoni mwa Mwaka 2024," David Axiotis, naibu meneja mkuu wa soko la China wa Kundi la Messe Berlin GmbH amesema.
Shanghai ilipokea wageni karibu milioni 1.9 kutoka Januari hadi Aprili mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 205 mwaka hadi mwaka.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma