Lugha Nyingine
Cameroon yafanya maadhimisho ya 52 ya Siku ya Taifa kwa magwaride ya kijeshi na kiraia (3)
Vikosi vya ulinzi vikishiriki kwenye gwaride wakati wa sherehe ya siku ya taifa ya Cameroon mjini Yaounde, Cameroon, Mei 20, 2024. (Picha na Kepseu/Xinhua) |
YAOUNDE - Cameroon imefanya maadhimisho yake ya 52 ya Siku ya Taifa Jumatatu kwa kufanya magwaride ya kijeshi na kiraia nchi nzima ambapo katika mji mkuu wa Yaounde, Rais wa nchi hiyo Paul Biya aliongoza sherehe hiyo iliyoshuhudia mamia ya wanajeshi na raia wakipita mbele ya viongozi wa kitaifa na kimataifa.
Maandamano yalifanyika katika mikoa yote 10 ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na maeneo ya watu wanaotumia lugha ya Kiingereza yanayokumbwa na vita, ambako wapiganaji wanaotaka kujitenga walikuwa wameweka kizuizi ili kuvuruga sherehe hizo.
Mei 20 ya kila mwaka ni moja ya siku muhimu zaidi nchini Cameroon. Tarehe hiyo Mwaka 1972, Wacameroon walipiga kura ya maoni ya kitaifa kwa ajili ya kuwa na nchi yenye umoja badala ya serikali ya shirikisho la majimbo iliyokuwepo wakati huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma