Lugha Nyingine
Wanaanga wa China wa?chombo cha Shenzhou-17 wakamilisha makabidhiano?na?kurudi?duniani kesho, tarehe 30 Aprili
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga ya juu cha Beijing Aprili 26, 2024 ikionyesha wanaanga wa chombo cha Shenzhou-17 na wale wa chombo cha Shenzhou-18 wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Jin Liangkuai)
JIUQUAN – Wanaanga wa China wa chombo cha Shenzhou-17 wamefanya makabidhiano na wanaanga wenzao wa chombo cha Shenzhou-18 na kukabidhi funguo za kituo cha anga ya juu cha China cha Tianhe kwa wanaanga hao siku ya Jumapili.
Hadi sasa, wanaanga hao wa chombo cha Shenzhou-17 wamekamilisha kazi zote zilizopangwa. Wanaanga hao watatu watarudi duniani kupitia kwenye eneo la kutua la Dongfeng katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China kesho Jumanne, Aprili 30, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China.
Kwa sasa, eneo hilo la kutua na mifumo yote inayoshiriki inafanya maandalizi ya mwisho kuwakaribisha wanaanga hao kurudi dunia.
Wanaanga hao wa chombo cha Shenzhou-17, ambao ni Tang Hongbo, Tang Shengjie na Jiang Xinlin, walifika kwenye kituo cha anga ya juu cha China cha Tianhe mwezi Oktoba mwaka jana, na wameendelea kuishi kwenye obiti kwa takriban nusu mwaka.
China ilirusha chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-18 tarehe 25 Aprili, na kutuma wanaanga watatu -- Ye Guangfu, Li Cong na Li Guangsu -- kwenye kituo cha Tianhe kwa ajili ya jukumu lingine la miezi sita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma