Lugha Nyingine
Wanaanga wa China wanaosafiri na chombo cha Shenzhou-18 waingia kwenye kituo cha anga ya juu
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga ya juu cha Beijing Aprili 26, 2024 ikionyesha wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-17 na wenzao wa chombo cha Shenzhou-18 wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Jin Liangkuai)
BEIJING - Wanaanga watatu wanaosafiri kwa chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou-18 wameingia kwenye kituo cha anga ya juu cha nchi hiyo cha Tianhe na kukutana na wanaanga wengine watatu siku ya Ijumaa, wakianza kupokezana zamu kwa wanaanga kwenye obiti.
Chombo hicho cha Shenzhou-18 kilichopeleka wanaanga hao watatu kwenye kituo cha anga ya juu cha China kutekeleza kazi ya muda wa miezi sita, kikiwa juu ya roketi ya Long March-2F, kiliruka majira ya saa 2:59 usiku (Kwa saa za Beijing) siku ya Alhamisi kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China.
Wanaanga wa chombo cha Shenzhou-17 walifungua kituo hicho saa 11:04 asubuhi (Saa za Beijing). Wanaanga hao ambao wamekuwa wakiishi kwenye kituo hicho waliwasalimu wanaanga wapya, na kupiga picha ya pamoja.
Kukutana kwa wanaanga wa vyombo hivyo viwili kumeanzisha mzunguko wa nne wa kupokezana zamu kwa wanaanga wa China wakiwa katika obiti kwenye kituo cha anga ya juu cha China.
Kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China, wanaanga hao sita wataishi na kufanya kazi pamoja kwa siku takriban 5 ili kukamilisha kazi zilizopangwa na kazi ya makabidhiano.
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga ya juu cha Beijing Aprili 26, 2024 ikionyesha wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-17 wakisalimia wenzao wa chombo cha Shenzhou-18 kwenye kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Jin Liangkuai)
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga ya juu cha Beijing Aprili 26, 2024 ikionyesha wanaanga wa ujumbe wa Chombo cha Shenzhou-17 wakisalimia wenzao wa chombo cha Shenzhou-18 kwenye kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Jin Liangkuai)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma