Lugha Nyingine
Eneo Kuu la Viwanda la Dongguan nchini China lashuhudia ukuaji wa biashara ya nje katika robo ya kwanza, 2024
Mtafiti akiendesha vifaa kwenye maabara ya teknolojia ya kasi ya masafa ya redio ya China Spallation Neutron Source (CSNS) huko Dongguan, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Julai 18, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)
GUANGZHOU - Katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2024, biashara ya nje ya Dongguan, eneo kuu la viwanda katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, ilifikia yuan bilioni 289.13 (dola za kimarekani bilioni 40.7), ikiendelea kushika nafasi ya pili katika mkoa huo wa Guangdong, viongozi wa eneo hilo wamesema.
Kiwango cha ukuaji wa biashara ya uagizaji na uuzaji bidhaa ya eneo hilo kilikuwa cha juu zaidi ikilinganishwa na kipindi kama hicho tokea Mwaka 2022, kikifikia ongezeko la asilimia 0.6.
Katika kipindi hicho, mauzo ya nje ya Dongguan ya soketi fungamani na moduli onyeshi za paneli bapa yaliongezeka kwa asilimia 5.2 na asilimia 24.2, mtawalia.
Wakati huo huo, asilimia zaidi ya 80 ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ni bidhaa za mitambo na umeme, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.5. Miongoni mwao, soketi fungamani zilizoingizwa kutoka nje ziliongezeka kwa asilimia 7.5.
Biashara ya eneo hilo na masoko yanayoibukia kama vile India, Brazili na Afrika Kusini iliongezeka kwa kasi kwa asilimia 8.9, asilimia 15.6 na asilimia 45.8 mtawalia.
Aina mpya za biashara ya nje za Dongguan zilikua kwa kasi, huku mauzo ya nje ya ununuzi wa moja kwa moja wa kuvuka mipaka na mauzo ya nje ya biashara ya mtandaoni yakiongezeka kwa asilimia 26.1 na asilimia 565.8 mtawalia.
Mwaka jana, uagizaji na uuzaji bidhaa wa Dongguan ulipata ongezeko tena tokea mwezi Oktoba, na kufanya jumla ya thamani ya biashara ya nje ya mwaka kufikia yuan trilioni 1.28.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma