Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China ahimiza Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China kutumikia?vema sera ya ufunguaji mlango
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitembelea mabanda ya kampuni mbalimbali kwenye Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 18, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)
GUANGZHOU - Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China yanapaswa kutoa mchango mkubwa zaidi katika kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa China na kuhimiza kujenga uchumi wa Dunia ulio wazi, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema siku ya Alhamisi alipotembelea eneo la maonyesho ya historia ya Maonyesho hayo huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China.
Waziri Mkuu Li, pia alitembelea mabanda ya kampuni mbalimbali kwenye Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China yaliyoanza Jumatatu wiki hii.
Waziri Mkuu Li amehimiza kampuni kuendelea kuboresha uwezo wao wa utafiti na maendeleo, na kujitahidi kuleta mageuzi ya kidijitali, akili bandia na ya kijani.
Kampuni zinapaswa kutumia kwa kutosha fursa kutoka kwenye Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China ili kuongeza umaarufu wa chapa za China na kuongeza biashara ya nje,” Waziri Mkuu Li amesema.
Kwenye kongamano na wawakilishi wa kampuni zinazoshiriki maonyesho hayo ya mwaka huu, Waziri Mkuu Li ameelezea matumaini yake kwamba kampuni zinazojikita katika biashara ya nje zitafanya juhudi zaidi kufuatilia soko la kimataifa, kuongeza ubora na thamani ya ziada ya bidhaa zao, na kushiriki katika uundaji wa vigezo vya kimataifa.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza na wawakilishi wa kampuni zinazoshiriki kwenye Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 17, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma