Lugha Nyingine
Tembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi | Magari ya "Made in China" yaoneshwa kwa umma (6)
Magari yanayotumia nishati mpya yakionyeshwa kwenye Banda la Maonyesho la Mkoa wa Jiangsu, China. (People’s Daily Online/ Niu Liangyu) |
Maonyesho ya 4 ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China yameanza Aprili 13 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Hainan, China. Kwenye eneo la maonyesho ya bidhaa za China na bidhaa ambazo zinafuatiliwa sana, mabanda ya maonyesho ya sehemu mbalimbali za mikoa ya China kama vile Guangdong, Guangxi, Chongqing, Shaanxi, Jiangxi, Zhejiang, Jiangsu, Jilin, na Hubei zimekuja na "hazina zao maalum za maajabu", na magari mengi ya "Made in China" yanaonekana papo hapo kwa umma.
Magari ya kuruka angani, magari ya michezo ya kutumia nishati mpya, magari ya kutumia teknolojia za kisasa, magari ya kubebea mizigo, pikipiki na aina nyingine zote yameonekana kama vivutio, ambavyo vinafuatiliwa na watazamaji wengi na kuwafanya wang'ang'anie huko kutazama. Magari ya "Made in China" yanaonyesha nguvu ya bidhaa na hamasa thabiti.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma