Lugha Nyingine
Maonyesho ya 4 ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China kuanza mkoani Hainan siku ya Jumamosi
HAIKOU - Maonyesho ya nne ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China yatafunguliwa kesho Jumamosi huko Haikou, mji mkuu wa Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China ambapo maonyesho hayo ya siku sita yatapokea chapa zaidi ya 4,000 kutoka nchi na maeneo 71, ambazo zinatarajiwa kuonyesha bidhaa bora na zinazohitajika sokoni kwa watumiaji wa kimataifa.
Eneo la ukumbi mkuu wa maonyesho hayo litafikia ukubwa wa mita za mraba 100,000. Eneo la maonyesho mengine kwenye sehemu mbalimbali katika kituo hicho ni lenye ukubwa wa mita za mraba 28,000, ambapo yatakuwa na maonyesho kuhusu hali mpya ya matumizi katika manunuzi ya vitu, na matumizi kwa ajili ya afya.
Nchi ya Ireland itakuwa mgeni wa heshima kwenye maonyesho hayo ya mwaka huu, ikiwa na ukumbi maalum wa maonyesho unaoonyesha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, elimu, uwekezaji, utalii na utamaduni wa nchi hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma