Lugha Nyingine
Njia ya Kupitisha Nishati ya Mashariki ya China Yafanyiwa Ukaguzi
Kuanzia tarehe 4 hadi 15 Aprili, laini ya umeme ya ±800KV ya Jiansu ya China itakuwa ikifanyiwa kazi ya ukaguzi na ukarabati wa kila mwaka. Kupitia ukarabati huo wa pande zote, kiwango cha uhakika wa usambazaji umeme wa laini hiyo kitaboreshwa zaidi.
Laini hiyo ya umeme ya Jiansu ni moja kati ya njia kuu za mradi wa "kupitisha umeme kutoka magharibi kwenda mashariki" nchini China, ambayo ina urefu wa kilomita 2,080 na inapita mikoa na miji mitano ya Sichuan, Chongqing, Hubei, Anhui, na Jiangsu. Kila mwaka mradi huo unaweza kusafirisha nishati safi ya umeme zaidi ya bilioni 30 kilowati-saa kwa mkoa wa Jiangsu.
(Picha na Du Yu/Xinhua)
Watu wakitazama kupatwa kwa jua kikamilifu kote Amerika Kaskazini
Shughuli ya kuadhimisha Siku ya Mashua ya Qintong 2024 yafanyika Jiangsu, China
Watu watoa heshima kwa marehemu kabla ya siku ya Qingming katika Mji wa Beijing, China
Msanii wa Ethiopia abuni sanaa kutokana na ufunuo wa kitabu maarufu cha China “Yi Jing”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma