Lugha Nyingine
Meli ya Xuelong 2 iliyo ya kwanza ya China ya kuvunja barafu kwenye ncha ya Dunia yatembelea Hong Kong (3)
Meli ya Xuelong 2 ya China ya kuvunja barafu kwenye ncha ya Dunia ikiingia kwenye Gati la Bandari huko Tsim Sha Tsui, Hong Kong, kusini mwa China Aprili 8, 2024. (Xinhua/Lui Siu Wai) |
HONG KONG - Meli ya Xuelong 2 iliyo ya kwanza kuundwa na China ya kuvunja barafu kwenye ncha ya Dunia, imewasili katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) wa China siku ya Jumatatu asubuhi kwa mara ya kwanza kufanya ziara ya siku tano huko baada ya kukamilisha utafiti wake mpya katika Bahari ya Antaktika.
Akizungumza katika hafla ya kukaribishwa kwa meli hiyo, John Lee, ofisa mtendaji mkuu wa Hong Kong, amesema kuwa meli ya Xuelong 2 ambayo imeingia kwenye gati la bandari huko Tsim Sha Tsui, Hong Kong, ni meli ya kwanza ya iliyoundwa na China ya kuvunja barafu kwenye ncha ya Dunia kwa ajili ya kufanya utafiti huko, kazi ya kuundwa kwa meli hiyo ni yenye uvumbuzi wa teknolojia kadhaa muhimu.
Lee amesema kuwa kituo cha kwanza cha safari ya kurudi nyumbani kwa meli ya Xuelong 2 ni mkoani Hong Kong ambapo timu ya watafiti wa Bahari ya Antaktika wa China itawasilisha kwa umma kazi zao na matokeo ya utafiti wa kisayansi, ikionyesha vya kutosha serikali kuu ya China inavyoijali Hong Kong.
Sun Shuxian, Naibu Waziri wa Maliasili wa China, amesema kuwa katika wakati timu ya watafiti wa China itafanya utafiti wa 21 katika Bahari ya Antaktika mwezi Oktoba mwaka huu, meli ya Xuelong 2 ya China ya utafiti wa ncha ya Dunia inatembelea Hong Kong na kukaribishwa kwa furaha.
Baada ya miaka 20, meli ya Xuelong 2 itaendelea na mawasiliano na ushirikiano kati ya taasisi za utafiti wa kisayansi za China Bara na Hong Kong katika nyanja ya utafiti wa ncha ya Dunia, Sun amesema.
Zhang Beichen, mwanasayansi mkuu ambaye ni kiongozi wa timu ya China ya utafiti wa 40 kwenye Bahati ya Antaktika amesema meli ya Xuelong, meli ya Xuelong 2 na meli ya mizigo ya Tianhui ziliondoka Shanghai Novemba 1, 2023 na kukamilisha kwa mafanikio kazi mbalimbali za utafiti zilizofanywa kwa siku 161 na kusafiri umbali wa jumla ya maili 81,000 baharini.
Kamati ya maandalizi ya ziara hiyo ya meli ya Xuelong 2 imetumai kuwa ziara hiyo itaongeza uelewa wa watu wa Hong Kong juu ya utafiti wa China kwenye ncha ya Dunia, haswa kuwawezesha vijana kuongeza hamu na shauku juu ya utafiti wa kisayansi wa ncha ya Dunia.
Shughuli ya kuadhimisha Siku ya Mashua ya Qintong 2024 yafanyika Jiangsu, China
Watu watoa heshima kwa marehemu kabla ya siku ya Qingming katika Mji wa Beijing, China
Msanii wa Ethiopia abuni sanaa kutokana na ufunuo wa kitabu maarufu cha China “Yi Jing”
Treni yaendeshwa katikati ya maua karibu na sehemu ya Juyongguan ya Ukuta Mkuu wa Beijing
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma